This archive report was first published on 10 October 2019.
Leo, Oktoba 10, 2019, familia ya mama na mwanawe waliozama baharini watakuwa na wakati mgumu wa kujua kwamba miili ya wapendwa wao itapatikana.
Wanafamilia wa Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walizama bahari mnamo Septemba 29, na kufunguliwa kwa pango majini Jumatano Oktoba 9, kwenye urafu wa mita 58 kwenda chini, likiwa limekwama kwenye pango matopeni.
Alhamisi, Oktoba 10, gari hilo litatolewa kulingana na msemaji wa serikali, Cyrus Oguna. Oguna alisema kundi la wapiga mbizi ambao wamekuwa wakizama majini kulitafuta gari hilo hatimaye waliweza kulipata na kuhakikisha kuwa ni lililokuwa na Mama Mariam.
"Tumehakikisha kuwa nambari za usajili za gari hilo ni KCB 289C ambazo ni sawia na zile za gari linalotafutwa. Tumeangalia pia kwenye CCTV na kuona kuwa ndilo hilo lilikuwa kwenye feri," alisema Oguna.
Shughuli za kulitoa gari hilo zitaanza mwendo wa saa tatu asubuhi Alhamisi, Oktoba 10.