Skip to main content

Mwanamuziki Eko Dydda ameona cha mtema kuni baada ya kumwunga mkono McDonald Mariga

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 October 2019.

Published on October 9, 2019, Mwanamuziki wa nyimbo za Injili Eko Dydda ameona cha mtema kuni baada ya kumwunga mkono mwanasoka McDonald Mariga katika kinyanganyiro cha kiti cha ubunge cha Kibra.

Alisema kuwa Mariga hatakuwa kama wanasiasa wengine ambao wakichaguliwa huwa hawatekelezi majukumu yao, lakini wao huwatelekeza wananchi waliowapigia kura.

Wafuasi wake walimkemea Dydda huku baadhi yao wakimtaka ajishughulishe na masuala ya kimziki na sio siasa.

Wengine hawakukosa kumvua nguo kwani walimtaka atafute suluhu kwa ndoa yake inayoyumbayumba kabla ya kuwashauri ni kiongozi yupi wanapaswa kumchagua Kibra.

Alipokashifiwa miezi kadhaa kwa kumfurusha nyumbani kwake mkewe na wanawe wawili, baada ya kumpata mpenzi mpya, madai aloyakana vikali.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →