Skip to main content

Amri kuhusu SGR ni Shere Tupu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 9 October 2019.

Maandamano hayo yalifanywa Jumatatu katika Mombasa, baada ya chama cha wasafirishaji mashehena kwa njia ya barabara (KTA) kufichua kwamba amri ya kusimamisha kwa muda ilikuwa bado haijatekelezwa bandarini.

“Kufikia leo hii saa kumi na mbili jioni, Halmashauri ya Bandari (KPA) bado inasafirisha mizigo yote inayoelekea bara bila ya kuwapatia wenye mizigo hiyo uhuru wa kuchagua njia gani ya usafiri wangependa kutumia,” ilisema taarifa ya chama cha KTA wikiendi iliyopita.

Maandamano hayo yalikuwa na lengo la kushutumu serikali kuu kwa kuchezewa shere za serikali kwenye suala hilo.

Maafisa wa polisi walitubua maandamano hayo katika vuta nikuvute, na baadhi ya wakereketwa hao walikamatwa.

Matukio haya yanaendelea kuongeza chumvi kwenye dhana nzito kwamba viongozi wa kisiasa wa eneo hilo huenda ‘wamekosa meno ya kung’ata’ katika juhudi za utetezi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →