This archive report was first published on 8 October 2019.
Seneti ya Kenya imeamua kumkamata mara moja Gavana wa Machakos Alfred Mutua kwa kukosa kufika mbele ya kamati ya uhasibu kuhusu bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2017/8.
Agizo hilo lilitolewa baada ya Mutua kukosa kufika mbele ya kamati hiyo Jumanne Oktoba 8, 2019, wakati alitarajiwa kujibu maswali ya kifedha.
Wakati huo, Mutua alijitetea kwa kusema kwamba alikosa kufika mbele ya kamati hiyo kwani seneta wa Machakos Boniface Kabaka alikuwa ameandaa kundi la vijana tayari kumkemea gavana akiingia kwenye kikao hicho.
Aliitaka kamati hiyo kufanya kikao kingine na kuhakikisha kuwa seneta Kabaka hahudhurii haki akidai kuwa seneta huyo ataleta tu siasa kwenye mjadala.
"Seneta Kabaka hafai kutumia kamati hiyo kwa maslahi yake," Mutua alisema.
Agizo la kukamatwa kwake lilitolewa na mwenyekiti wa kamati ya Uhasibu bungeni Moses Kajwang'.
Alisema kwamba kamati hiyo imemtaka Mutyambai kumkamata Mutua na afikishwe mbele ya kamati hiyo ili ajibu maswali ya kifedha ya mwaka wa 2017/18.
Alisema pia kwamba si mara ya kwanza kwa gavana huyo kutofika mbele ya kamati hiyo na hivyo agizo la kukamatwa kwake kutolewa.