This archive report was first published on 8 October 2019.
Maafisa wa polisi nchini India wamepata zaidi ya KSh 1 milioni kwenye nyumba ya ombaomba mmoja aliyeaga dunia kutokana na ajali ya barabarani Ijumaa, Oktoba 4.
Ombaomba huyo, Azad, alikuwa akiishi pekee yake katika mtaa duni kule Govandi nchini India.
Alifariki dunia baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani.
Maafisa wa polisi waliweza kupata zaidi ya KSh 1 milioni kwenye nyumba ya Azad baada ya kuhesabu sarafu alizokuwa akikusanya kwa muda wa saa nane.
Polisi waliweza pia kupata kitambulisho chake na sitakabadhi kadhaa zilizowawezesha kumtambua kwa haraka.
Hivi sasa, polisi wameanza juhudi za kuitafuta familia yake huku fedha hizo zikiwekwa kwenye benki wakisubiri kuipata familia.