Skip to main content

Waziri Fred Matiang'i Kuridhika na Vita dhidi ya Kampuni za Kamari

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 7 October 2019.

Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang'i, amesema kuwa hakuna taifa duniani lililojengwa kwa mchezo wa kamari na atakapofaulu, hakutashitisha vita hivyo.

Alisema hivyo wakati alihudhuria mkutano wa viongozi wa dini ya Kiislamu katika musikiti wa Jamia mnamo Jumatatu, Oktoba 7, 2019.

Waziri Matiang'i alisema kuwa operesheni hiyo ilikuwa imeanza kuzaa matunda na hatalegeza kamba hadi atakapofaulu.

"Hakuna nchi iliyojengwa kupitia kucheza kamari, na kwa hivyo nina wahimiza Wakenya kuunga mkono operesheni hii," alisema Matiang'i.

Operesheni hiyo ilipelekea kufungwa kwa kampuni mbili kuu za kamari, Sportpesa na Betin, baada ya serikali kuanza kutoza ushuru wa 20% katika kila ushindi.

Waziri wa Wengi Bunge la Kitaifa, Aden Duale, alisema mchezo wa kamari unatakiwa kupigwa marufuku kwani ni tishio kwa usalama wa taifa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →