Skip to main content

Mbunge Ngunjiri Wambugu adai viongozi wa Mlima Kenya wako tayari kumnunua Raila

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 7 October 2019.

Wambugu alisema hili baada ya mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria kudai kuwa Raila hana umaarufu eneo la Mlima Kenya na hata hawezi akapigiwa kura na wakazi.

Wambugu alipinga madai ya Kuria kwamba Raila hawezi akapata kura zozote eneo la Mlima Kenya na kwamba kundi la Kieleweke limekuwa likimfanyia kampeni kiongozi huyo wa chama cha ODM.

Wambugu alisema kuwa Raila anaweza akanunuliwa kwa haraka sana na viongozi wa eneo la Mlima Kenya ikizingatiwa kuwa naibu Rais William Ruto alinunuliwa pia miaka mitano iliyopita na ni Uhuru aliyemuuza katika eneo hilo.

Wambugu alisema, "Nikisikia watu wengine wakisema kwamba Raila hawezi akauzwa eneo la Mlima Kenya, nacheka tu, ninakumbuka Ruto alivyonunuliwa miaka mitano iliyopita na ni Uhuru aliyemuuza katika eneo hilo," Wambugu alisema.

Wambugu alisema kuwa kwa sasa tunamtazamia Uhuru tena, akiamua kumuuza Raila kwetu sisi, tutamnunua kwa asilimia 100%, tukikumbuka kwamba alituuzia Ruto hata kama hajakuwa Rais," Wambugu alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →