Skip to main content

Wabunge Wanawake Wataka Serikali Kukabiliana na Uzoefu wa Mariam na Amanda

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 7 October 2019.

Wabunge Wanawake Wataka Serikali Kukabiliana na Uzoefu wa Mariam na Amanda

Wabunge wanawake kutoka Chama cha Jubilee wameikashifu serikali kwa kuchelewa kuopoa miili ya Mariam Kigenda, mwenye umri wa miaka 35, na mwanawe Amanda Mutheu, mwenye miaka minne, ambao gari lao lilitumbukia baharini mnamo Jumapili, Septemba 29, 2019, wakiwa wakiwa kwenye feri MV Harambee katika kivukio cha Likoni.

Wabunge hao wakiongozwa na Aisha Jumwa, Mwakilishi wa akina Mama Nakuru Susan Kihika, na Mbunge wa Kandara Alice Wahome, wameitisha kambi katika kivukio cha feri Likoni wakati wa sherehe ya Mashujaa, endapo miili ya mama na mwanawe waliotumbukia Bahari Hindi haitapatikana.

“Endapo miili hiyo haitaopolewa, nitawaongoza akina mama kutoka kote nchini kukutana Likoni wakati wa siku kuu ya Mashujaa kuomboleza kifo cha Kigenda na mwanawe,” alisema Jumwa.

Matamshi yao yaliungwa mkono na Wakenya waliojawa na ghadhabu, ambao waliibua ghathabu zao dhidi ya serikali kwa kutumia heshi tegi #BoycottMashujaaDay kwenye mtandao wa Twitter.

Wanawake hao pia wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuwafuta kazi maafisa wakuu wa Huduma za Feri Kenya (KFS) kwa kukosa kudumisha usalama wa mamilioni ya Wakenya ambao hutumia feri kila siku.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →