This archive report was first published on 7 October 2019.
Seneta Millicent Omanga, mmoja wa viongozi wa kike wa kundi la Inua Mama, alikuwa na umbo lake la kuvutia wakati wa mkutano wa kundi hilo eneo la Kandara.
Alipofika kwenye mkutano, Omanga alijilegeza na kisha kusakata ngoma huku akitingisha umbo lake la kuvutia na kufanya wafuasi wake kuzama kwenye fikri za matamanio.
Video ya mkutano huo ilikuwa na umuhimu mkubwa kwa wafuasi wake, ambao walitamani wawe na umbo kama hilo la kuvutia wakisakata densi.
Omanga hujivunia umbo lake licha ya kuwa munene kiasi, na kuna wakati amewahi kiri kwamba anayapenda makalio yake kupindukia.
Alipokata kiuno, Omanga alionyesha umahiri wake katika sekta hiyo, na kuwaacha viongozi wenzake wakishangaa alijulia wapi kusakata densi za kisasa.
Video hiyo iliwafurahisha wafuasi wake, na kuonyesha kuwa Omanga ni mmoja wa viongozi warembo kwenye mabunge ya kitaifa.