This archive report was first published on 6 October 2019.
Wakati wa Siku ya Walimu Ulimwenguni mnamo Oktoba 6, 2019, gazeti la Uingereza la The Independent lilimsifu Peter Tabichi kwa juhudi zake za kuboresha maisha ya wanafunzi.
Tabichi, mwalimu kutoka Kenya, sasa yuko nchini Uingereza kufanya mkutano na viongozi na mashirika zisizokuwa za serikali.
Chapisho hilo lilimsifia Tabichi kwa kazi yake ya ukarimu na kutokuwa mbinafsi, ambayo imefanya shule yake iliyokuwa na rasilimali duni kuibuka bora baada ya kushinda mashindano ya sayansi ya kitaifa.
Tabichi alikuwa miongoni mwa walimu waliopongezwa kwa kazi yao tofauti katika sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Alijipatia nafasi ya kuhutubu katika Baraza Kuu la 74 la Umoja wa Mataifa jijini New York mwezi Septemba, na kabla ya hayo, alitembelea Ikulu ya White House ambapo alikutana na Rais wa Marekani Donald Trump.
Stephanie Grisham, karani wa habari katika Ikulu ya White House, alimsifia Tabichi kama mwanamume mwenye bidii ambaye amejitolea sana katika taaluma yake ili kutoa huduma kwa binadamu.