This archive report was first published on 6 October 2019.
Mbunge wa Gatundu Kusini, Moses Kuria, amesema kuwa serikali inatoa ahadi za uwongo kwa Wakenya kuhusu miili ya Mariam na Amanda, ambayo imenaswa chini ya Bahari Hindi kwa siku nane.
Alisema hili katika ujumbe aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo Jumamosi, Oktoba 5.
"Shirika la Huduma za Feri (KFS) liwache kupea Wakenya matumaini ya kuwa wataopoa miili na gari. Dakika saba zilipotezwa wakitazama mama na mwanawe wakifa maji. Tuangazie kwa kufuta kazi Afisa Mkuu Mtendaji na kuhakisha kuwa haya hayatajirudia tena," aliandika mbunge huyo.
Alijiunga na wabunge wengine ambao pia wanataka maafisa wakuu wa KFS wafutwe kazi kufuatia mkasa wa kivukio cha Likoni ambao ulifichua udhaifu wa serikali kukabiliana na majanga.
Wabunge hao waliwaelekezea kidole cha lawama mkurugenzi mkuu Bakari Gowa na Meja Generali wa Jeshi la Wanamaji Franklin Mghalu baada ya wafanyakazi wao kushindwa kuwaokoa wawili hao licha ya kituo chao kuwa karibu na kulipotokea mkasa huo na pia kukosoa wajibu wa Kenya Coast Guard.
"Tulipitisha sheria hivi majuzi ya kubuni Kenya Coast Guard. Wajibu wao ni kutoa huduma za usalama katika safari za majini. Tunataka kujua kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Brigadier Vincent Loonena walipokuwa na walichokuwa wakifanya," ilisoma taarifa ya wabunge hao.
Alipitisha taarifa hii mnamo Oktoba 1.
Alisema kuwa serikali inatoa ahadi za uwongo kwa Wakenya kuhusu miili ya Mariam na Amanda, ambayo imenaswa chini ya Bahari Hindi kwa siku nane.
Alisema hili katika ujumbe aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mnamo Jumamosi, Oktoba 5.
Alisema kuwa serikali inatoa ahadi za uwongo kwa Wakenya kuhusu miili ya Mariam na Amanda, ambayo imenaswa chini ya Bahari Hindi kwa siku nane.