This archive report was first published on 6 October 2019.
Kamanda: DP Ruto Anatumia Pesa Za Wizi Kushawishi Wapiga Kura ¶
Uchaguzi wa Kibra unaonekana kugeuka kuwa uwanja wa kupimana nguvu kati ya Ruto na Raila.
Mbunge mteule wa Jubilee Maina Kamanda amesema DP Ruto anatumia pesa za wizi kushawishi wapiga kura katika uchaguzi wa Kibra.
Alisema hilo halitafaulu na kuwataka wanaKibra kupiga kambi kwa Ruto lakini debeni wapatie Okoth kura.
Uchaguzi huo mdogo wa Kibra, ambao ulisababishwa na kifo cha aliyekuwa mbunge wa ODM Ken Okoth, umegeuka kuwa uwanja wa Raila kutoana kijasho na hasimu wake wa kisiasa DP Ruto.
DP Ruto amekuwa akiongoza kampeni za McDonald Mariga kuchukua kiti cha ubunge cha Kibra.
Alisema kiti hicho kitaenda kwa mgombea wa Jubilee kwa sababu wakazi walichoshwa na siasa za Baba.
Alisema hilo halitafaulu na kuwataka wanaKibra kupiga kambi kwa Ruto lakini debeni wapatie Okoth kura.
Alisema Ruto lazima aibike kwa watadunda na Mariga kwenye uchaguzi huo mdogo utakaofanyika Novemba saba.
Alisema Ruto anatumia mamilioni ya pesa kukoroga siasa za Nairobi katika kile alisema ni kuhujumu mwafaka wa handisheki.
Alisema sisi tunajua Okoth, kwa sababu ya handisheki tumepata amani hii Nairobi.
Alisema wakati hatukuwa na handisheki Nairobi kazi haikuwa inafanyika, mimi niko na biashara Nairobi na sikuwa nafungua... nyumba zangu Mathare hazikuwa zinalipwa.
Alisema huko Karen mkiitwa endeni, fanyeni huko mkahawa na mkule hizo pesa kwa sababu ni zile mnaskia zimeibwa.
Alisema mkiitwa watu mia moja endeni watu elfu tatu mchukue hiyo pesa... hiyo ni mkahawa.