Skip to main content

Boni Khalwale Omboleza Mkewe wa Kwanza Adelaide Khalwale

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 5 October 2019.

Boni Khalwale Omboleza Mkewe wa Kwanza Adelaide Khalwale

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale ameomboleza kifo cha mkewe wa kwanza Adelaide Khalwale ambaye alifariki akiwa katika makazi yao eneo la Malinya, kaunti ya Kakamega.

Adelaide alifariki Jumamosi, Oktoba 5, 2019, baada ya kupata matatizo ya kupumua, kinyume cha habari ambazo zilikuwa zimefichuliwa kwa umma kwamba alifariki kutokana na saratani.

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale alisema marehemu alifariki kutokana na matatizo ya kupumua na kupuzilia ripoti za awali kwamba alifariki kutokana na saratani.

Adelaide alikuwa akihudumu katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknologia cha Masinde Muliro, kaunti ya Kakamega, hadi kifo chake.

Aliyekuwa seneta wa Kakamega Boni Khalwale aomboleza kifo cha mkewe wa kwanza, Adelaide Khalwale. Picha: Boni Khalwale/ Facebook

"Ili kuondoa shauku, ningependa kutangaza kuwa mke wangu ambaye tumeoana kwa miaka 39 amefariki. Mwaka wa 2003 alipatikana na saratani ya mfuko wa kizazi na akapona. Siku mbili zilizopita alikumbwa na matatizo ya kupumua na leo asubuhi tumempoteza," alifichua Khalwale.

Naibu Rais William Ruto na seneta wa Bungoma Moses Wetangula walikuwa wamejumuishwa na wakenya katika kutuma risala zao za rambirambi kwa familia ya marehemu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →