Skip to main content

Ajuza wa Mau Mau Amlilia Rais Uhuru Kenyatta Kumsaidia

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 4 October 2019.

Barabara ya kwenda kwake nyumbani katika kaunti ya Nyeri, ambayo ni sehemu ya kijiji chake, imeharibika na kufanya maisha yake ya ufukara kuwa zaidi ya kawaida.

Alisema alikuwa mmoja wa wale walioingia msituni wakati wa vita vya Mau Mau kupigania uhuru wa nchi hii na baada ya uhuru kupatikana, rais wa kwanza Mzee Jomo Kenyatta alikuwa ameahidi kukutana naye.

"Wakati wa vita dhidi ya wakoloni, nilipata kichapo hivi kwamba siwezi kusimama. Na ninapopelekwa hospitali lazima nibebwe na barabara ni mbovu. Ndio naomba barabara hiyo itengenezwe," alisema.

Aliongeza, "Nimekuwa nikienda kwa kamishna na kuniambia kuwa atakuja kuunda lakini hajafanya hivyo. Tafadhali nisaidieni hii baraabara iundwe."

Aliteta kuwa licha ya kupigania uhuru ambao Wakenya wanafurahia kwa sasa, amekuwa akiishi maisha ya ufukara.

"Ningependa kukutana na Rais Uhuru na pia anisaidie ili hii barabara iweze kukarabatiwa," alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →