This archive report was first published on 4 October 2019.
Volker Bassen, mtaalam wa masuala ya kupiga mbizi kutoka Uswidi, amejiunga na kikosi cha Jeshi la Wana Maji katika oparesheni ya kuopoa miili ya waathiriwa wa mkasa wa Bahari Hindi.
Alhamisi, Oktoba 3, Bassen alitangaza kuwa anahitaji saa mbili tu kuiopoa miili ya Mariam Kigenda na mwanawe Amanda, ambao walikumbana na mauti baada ya gari lao kudondoka kutoka kwa feri na kutumbukia baharini katika kivukio cha feri Likoni Jumapili, Septemba 29.
Alipotangaza hili, Bassen alifichua kuwa ana vifaa maalum ambavyo atavitumia katika kubaini ni sehemu ipi haswa ambapo miili hiyo ipo kando na gari la waathiriwa.
Alipokubaliana na Bassen, Msemaji wa serikali Cyrus Oguna alisema kuwa atashirikiana na jeshi hilo kwenye oparesheni hiyo na kuwa tayari kuna wapiga mbizi baharini ambao wanapiga darubini maeneo ambayo tunahisi huenda miili hiyo ikawa.
Shirika la Feri limekuwa likitoa wito kwa Wakenya kuwa watulivu huku zoezi hilo likiendelea.
Wataalam walisema kuwa eneo lililoko gari hilo ni takriban mita 60 baharini humo ila shughuli nzima imetatizika kutokana na hali mbaya ya hewa.