Skip to main content

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali ataka Waziri wa Uchukuzi James Macharia ajiuzulu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 October 2019.

Waziri wa Uchukuzi James Macharia amejipata pabaya baada ya mkasa wa feri Likoni ambao ulisababisha kifo cha mama na mwanawe walioanguka kwenye Bahari Hindi. Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amemtaka Waziri wa Uchukuzi James Macharia ajiuzulu baada ya mkasa huo.

Ali alisema kisa hicho kilitokana na utepetevu kwenye wizara hiyo na hivyo mkuu wake lazima ang'atuke uongozini. 'Leo ni siku ya tatu tangu mkasa ufanyike, na hapo ndio uliona umuhimu wa kutuma katibu aje ashughulikie suala la kuitafuta miili hiyo,' alisema Ali.

Ali alisema pia wote ambao wanashikilia nyadhofa katika shirika la feri nchini pia wanafaa kujiondoa kwa utepetevu. 'Baada ya kujiuzulu, wanafaa wakamatwe ili waelezee ni kwa nini wamekosa kufanya kazi yao,' alisema.

Ali alizungiumza wakati ambapo wakenya wamegadhabishwa na utepetevu wa serikali katika kutafuta miili ya mwanamke na mwanawe waliozama kwenye Bahari Hindi Jumapili, Septemba 29.

Wanajeshi wa kitengo cha wanamaji wako kwenye maandalizi ya kuonyesha makali yao wakati wa sikukuu ya Mashujaa itakayofanyika majuma matatu yajayo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →