Skip to main content

Mwanabodaboda amfumania binamuye akifungua 'server' za mkewe mwenye mimba ya miezi 8 ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 3 October 2019.

Alhamisi, Oktoba 3, 2019, kijiji cha Nyakunguru, kaunti ya Nyamira, ilishuhudia sinema ya bure baada ya mhudumu wa bodaboda kumfumania mkewe ambaye ni mja mzito akila uroda na binamuye.

Wawili hao walikuwa wa jamii moja na marafiki wa dhati ambao mara kwa mara huonekana pamoja.

Basweti, ambaye anatambulika kama kijogoo, alisemekana kummezea mate mkewe Job, na kupeleka wawili hao kuanza uhusiano wa mapenzi ambao umekuwa ukiendelea kwa miezi.

Job alinong'onezewa na majirani kuhusu uhusiano wa mapenzi ambao ulikuwa unaendelea baina ya mkewe na binamuye.

Alipomuuliza mkewe kuhusu fununu hizo, mama alijitetea vikali na kusema kuwa hawezi akafanya mapenzi na mume mwingine ilhali alikuwa mja mzito tayari.

Job aliamua kufanya uchunguzi zaidi hadi Alhamisi alipowafumania wawili hao kitandani siku zao za arobaini zilipowadia.

Job ambaye ni mhudumu wa bodaboda kaunti ya Nyamira alipashwa na majirani kuwa mkewe alikuwa anachumbiana na binamuye.

Aliposhwa na majirani, Job aliingia katika chumba chao cha kulala kupitia dirisha na kuwafumania binamuye na mkewe kitandani mwake.

Job alitoka nje akipiga mayowe kuwaita majirani huku binamuye ambaye alihofia kichapo akihepa mara moja.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →