This archive report was first published on 2 October 2019.
Maandamano yalishuka kijiji cha Maseno, Subukia baada ya barubaru mmoja kuufukua mwili wa babake na kumvua viatu ili aviuze.
Alama ya kushuhudia kizaa ilikuwa Jumatano Oktoba 2, 2019, wakati jamaa huyo alifumaniwa asubuhi akiwa tayari ameufukua kaburi hilo ambapo babake alizikwa miaka 14 iliyopita.
Polisi walisema mshukiwa huyo, Patrick Mwangi Katonya, alisema alifukuza mwili huo ili kumvua viatu vya bei alivyokuwa amezikwa nazo babake.
"Mshukiwa aliambia polisi kuwa alitaka kuuza viatu alivyozikwa navyo babake. Alisubiri jamaa wa familia kuondoka nyumbani ndio akaanza shughuli za kuufukua mwili huo," polisi walisema.
Viati vimeoza vilikuwa kinyume cha kile mshukiwa alikuwa akilenga, na hivyo kusababisha kufungwa kwake hospitalini kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kushtakiwa.