This archive report was first published on 2 October 2019.
Mathew Knowles, babake mwanamuziki nyota Beyonce, amefichua kuwa anakabiliwa na saratani ya matiti. Hii ni taarifa muhimu ambayo inaleta wasiwasi kwa familia yake.
Mathew alisema alikumbwa na wasiwasi alipoona kila mara mashati yake na shuka yakigeuza rangi. Mkewe pia amekuwa akitambua damu kwenye kitanda chao kwa kipindi kirefu.
Mathew alifichua kuwa anakabiliwa na saratani ya matiti, ambayo inahatarisha maisha ya wanawe na wajukuu wake. Picha: TheSun
Mathew alisema alikata kauli ya kumtembelea mtaalam ambapo alifanyiwa uchunguzi. Knowles aliingiza baridi baada ya kuthibitishiwa alikuwa muathiriwa wa ugonjwa huo.
“Nina vitu vinne vya kunipa wasiwasi, saratani ya kibofu, saratani ya utumbo, melanoma na saratani ya matiti,” alisema mzee Knowles.
Mathew ambaye alikuwa meneja wa Beyonce, tayari amefanyiwa upasuaji na anaendelea kupona. Kwa sasa ana mtazamo tofauti na maisha na anapania kuwa wanaume wengi watajitokeza ili kupimwa ugonjwa huo.
“Nimetambua kuwa idadi ya wanaume ambao wanaugua saratani ni ndogo kwa sababu ni wachache ambao hujitokeza kupimwa,” aliongezea Mathew.