This archive report was first published on 2 October 2019.
Mapema Jumatano, Oktoba 2, 2019, Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho alijitokeza kuvunja kimya chake kwa kuwataka wakazi wa Mombasa kuwa watulivu baada ya ajali ya feri Likoni.
Ali Hassan Joho alisema kuwa familia na jamaa ya Mariam Kighenda, ambaye na mwanawe Amanda Mutheu walikufa maji baada ya gari lao kutumbukia baharini kwenye kivuko cha feri cha Likoni, Mombasa, walikuwa wakisubiri kwa uchungu huku shughuli za uokoaji ukiendelea.
Alisema kuwa operesheni hiyo ndio imechelewesha na kwa hivyo tunaomba subira. Tuna vikosi tofauti ambavyo vimehusika kwenye msako huo.
Gavana Joho pia alihimiza Shirika la Huduma za Feri (KFS), kuimarisha usalama kwa kuweka vizuizi vya kulinda magari vinavyoweza kukumbwa na hitilafu.
Shughuli za kutafuta miili hiyo inaendelea hii leo huku Msemaji wa Serikali Cyrus Oguna akisema kuwa wapiga mbizi wanatoka katika Jeshi la Wanamaji, Shirika la Huduma za Feri (KFS), taasisi ya utafiti wa baharini na Halmashauri ya Bandari Kenya (KPA).