This archive report was first published on 1 October 2019.
Wakenya wamegadhabishwa na utepetevu wa serikali katika kutafuta miili ya mwanamke na mwanawe waliozama kwenye Bahari Hindi Jumapili, Septemba 29.
Wanajeshi wa kitengo cha wanamaji walikuwa wakifanya maandalizi ya kuonyesha makali yao wakati wa sikukuu ya Mashujaa itakayofanyika majuma matatu yajayo.
Wanajeshi hao wanaonekana wakifanya mazoezi na kuonyesha ujuzi wao kwenye safu hiyo ya wanamaji, lakini miili ya Mariam na Amanda waliozama kama mita 100 kutoka wanapofanyia mazoezi bado haijapatikana.
"Wanajeshi wa maji wakifanya mazoezi katika bustani ya Mama Ngina, Mombasa. Hata hivyo, miili ya Mariam na Amanda waliozama kama mita 100 kutoka wanapofanyia mazoezi bado haijapatikana," alisema Crispus Alex.
Wakenya wengi wameudhi na kushangaa ni vipi kikosi hicho kitajishasha kwenye sherehe hizo ilhali hakuna juhudi za uokoaji zilizofanywa kuhakikisha maisha mama na mwanawe yameokolewa.
Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu walizama Jumapili, Septemba 29, wakati ambapo gari lao lilirudi nyumba baada ya kupakiwa kwenye feri.
Waliokuwepo walishuhudia wawili hao wakizama pasi la kufanya.
Wanajeshi wa kitengo cha wanamaji wakifanya maandalizi ya maonyesho ya siku ya Mashujaa. Picha: Crispus Ale