Skip to main content

Gari la Magereza Lapinduka Embu, Kuua Mfungwa na Kujeruhi Wengine

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 1 October 2019.

Gari la Magereza Lapinduka Embu, Kuua Mfungwa na Kujeruhi Wengine

Mapema Jumanne, Oktoba 1, 2019, gari la magereza lilipinduka eneo la Kathageri karibu na Daraja la Thuci, Kaunti ya Embu, na kuua mfungwa mmoja na kujeruhi wengine saba.

Askari watano wa magereza pia walipata majeraha wakati wa ajali hiyo na wote walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Chuka.

Afisa msimamizi wa Gereza la Embu, Henry Ochieng, alisema gari hilo lilipinduka mara kadhaa lilipokuwa kwenye mteremko.

"Ni huzuni tumempoteza mmoja wa wafungwa ambaye alikuwa akihudunia kifungo cha maisha jela. Wafungwa wengine na baadhi ya maafisa wetu walipata majeraha mbalimbali eneo la Kathageri. Barabara ni yenye mlima na dereva alishindwa kulidhibiti na kupunduka," Ochieng alisema na kunukuliwa na The Standard.

Aliongeza kwamba wafungwa hao walikuwa wakisafirishwa kutoka Gereza la Embu kwenda Mahakama za Meru.

Dereva wa gari hilo naye alijeruhiwa vibaya na kupelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Embu Level Five.

Maureen Mwende, mmoja wa walioshuhudia, alisema ajali hiyo ilitokea asubuhi ya 6:30am na mvua ilikuwa ikinyesha rasharasha.

"Dereva alishindwa kulidhibiti gari, nafikiri ni kutokana na barabara kuwa telezi," alisema.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →