This archive report was first published on 1 October 2019.
Timu ya BBI inatarajiwa kutoa ripoti yake kwa Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga, na kisha kundi la mawakili litatoa swali la kura ya maamuzi.
Hiyo ni kwa mujibu wa Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha Wiper, aliyekosoa michango ya Naibu Rais William Ruto kote nchini.
Alisema Ruto anazunguka nchini na pesa za ufisadi, na kuwakataa wale wanaosema michango yake ni kushabikia ufisadi.
"Wengine wanafikiria kwamba BBI italeta mapendekezo ya kubadili katiba, lakini sivyo. Wataleta ripoti tu kwa yule aliyewachagua," alisema Kalonzo.
Alizungumza kwenye mkutano wa wanachama wa Wiper katika afisi za chama chake jijini Nairobi, Jumatatu Septemba 30.
Alipigia kalamu kwa Naibu Rais William Ruto, akisema ni huzuni kwamba baadhi ya viongozi wanamwaga pesa kila siku na kutaka tuamini wanapiga hatua ilhali tunajua vizuri ni pesa za ufisadi.