This archive report was first published on 1 October 2019.
Mbunge wa Fafi AbdiKarim Osman amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kufufua uchunguzi kuhusu utajiri wa Aden Duale, ambaye anasema amepata utajiri mkubwa sana tangu aingie bunge.
Osman alisema kampeni hiyo inafaa kumlenga sana mbunge wa Garissa mjini Aden Duale, akisema kuwa amekuwa kiongozi mwenye kiburi kiwango cha kuwa anawaonyesha wengine dharau.
Alisema, "Kama Mungu amekubariki kiwango cha kuwa una ghorofa, usitumie hilo kuwatusi wanaume wengine. Duale sasa anamtusi Abbas...na kusema kuwa Garissa ni kwake. Kuna wanaume kutoka hii kaunti ambao wanaweza chukua hii kazi ya ubunge na kuifanya vizuri,"
Osman aliongeza kuwa kabla ya Duale kuchaguliwa bungeni mnamo mwaka wa 2007, alikuwa ni mtu hoi tu huku wakati mmoja akifanya kibarua cha broka kaunti ya Mombasa.
Aliongeza, "Mwaka wa 2002, Duale hakuwa na chochote sawa na mwka wa 2007. Baada ya kuchaguliwa mbunge 2008, alifika Nairobi kwa kupewa lifti,"