Skip to main content

Balozi wa Marekani ajipata taabani kwa kushutumu ufisadi Kenya

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 30 September 2019.

Balozi wa Marekani ajipata taabani kwa kushutumu ufisadi Kenya

Balozi wa Marekani nchini Kenya, Kyle McCarter, mnamo Jumapili, Septemba 29, alionja ghathabu ya Wakenya kwa kukashifu ufisadi nchini.

Alisema serikali inatakiwa kuchukua hatua ya dhidi ya wezi wakubwa ili kukabiliana na ufisadi.

McCarter alihudhuria hafla iliyokuwa imeandaliwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) na Idara ya Mahakama.

“Nilisimama na marafiki shupavu kukabiliana na wezi wanao wanyima wananchi haki ya kutekelezewa Agenda Kuu Nne. @USAMarafiki inahusika pakubwa kukabiliana na saratani ya wezi. Wezi wakubwa wanatakiwa kukamatwa,” aliandika McCarter.

Ujumbe wake haukuwafurahisha baadhi ya Wakenya ambao walitaka kujua hatua ambayo Marekani imechukua ili kuisaidia Kenya kukabiliana na visa vya ufisadi huku wengine wakimkashifu kwa kula pamoja na wafisadi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →