This archive report was first published on 29 September 2019.
Mwanariadha Braima Dabo, amiminiwa sifa kwa kumsaidia mwenzake aliyekaribia kuzimia kumaliza mashindano ¶
Braima Dabo, mwanariadha kutoka Guinea-Bissau, alimsaidia mwenzake Johnathan Busby kumaliza mashindano ya mita 5,000 jijini Doha, Qatar, mnamo Septemba 27, 2019.
Busby, ambaye alikuwa akishiriki mashindano ya riadha za dunia, alikuwa anakaribia kuzimia wakati Dabo alilazimika kumsaidia kumaliza mbio.
Telegraph inaripoti kuwa Busby alikuwa akikaribia kuzirai, lakini Dabo alilazimika kumburuta huku mwanariadha huyo akionekana akichechema hadi nyumbani huku mashindano yakiendelea kunoga ugani Khalifa.
Selemon Barega kutoka Ethiopia ndiye alikuwa mshindi wa mbio hizo kwa kumaliza kwa muda wa 13: 24.69.
Video ya mwanariadha huyo ambayo imekuwa ikisambaa mitandaoni, inawaonyesha wawili hao wakimaliza mbio hizo dakika tano baada washindani wenzao kumaliza mbio hiyo.
"Azma yangu ilikuwa kuiwakilisha taifa langu kwa njia bora na ninafuraha kuwa nilimsaidia mwenzangu," Dabo aliambia Reuters.
"Niliona hakuwa akikimbia kwa njia nzuri, alikuwa ameinama, nilitambua hangeweza kumaliza," Dabo aliongeza.
Selemon Barega kutoka Ethiopia ndiye alikuwa mshindi wa mbio hizo kwa kumaliza kwa muda wa 13: 24.69.