This archive report was first published on 29 September 2019.
Barabara ya Kisumu-Kisii ilikuwa imeharibika baada ya mvua kubwa kutokea, kusababisha mafuriko na kusomba daraja kwenye soko la Kodada eneo la Rachuonyo Mashariki, kaunti ya Hombay.
Wasafiri walitatizika kwa takriban saa kumi baada ya mafuriko kusomba daraja la soko la Kodada na kuathiri usafiri katika barabara ya Kisumu-Kisii.
Sehemu ya barabara hiyo ambayo ilikuwa imeharibika ilikuwa inakarabatiwa na kampuni ya Uchina, ambapo wasafiri walihisi kuwa ndicho chanzo cha kuathirika kwa daraja hilo.
Kamanda wa polisi Rachuonyo Mashariki, Charles Barasa, aliwashauri madereva kutumia njia mbadala, akionya kuwa eneo hilo huenda likaathirika zaidi na mafuriko kutokana na mvua inayozidi kunyesha.
Barasa aliogeza kuwa ujenzi wa daraja lingine unaendeshwa tayari baada lililokuwepo kusombwa na mafuriko.
"Madereva ambao hutegemea hii barabara hawapaswi kuitumia wakati wa mafuriko. Wanakandarasi wamewahakikishia wasafiri kwamba daraja lingine linaundwa ili kuepuka hatari inayoweza kusababishwa na eneo hilo," alisema Jumamosi, Septemba 28, 2019.