Skip to main content

Gavana Joho Aongeza Ada ya Kuzika Makaburini Mombasa

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 29 September 2019.

Gavana Joho Aongeza Ada ya Kuzika Makaburini Mombasa

Wakazi wa Mombasa wamekataa kuwazika wapendwa wao baada ya serikali ya kaunti hiyo kuongeza ada ya makaburi ya umma.

Ada ya kudumu imeongezwa kutoka 25,000 hadi 30,000 kwa mwaka, kama ilivyotajwa katika makadirio ya mwaka wa fedha wa 2019/2020.

Maeneo matatu ya makaburi ya umma yameletwa katika kaunti ya Mombasa, ikiwemo Kisauni, Mbaraki, na Mayimbo.

Wakazi wamekataa hatua hiyo, kusema kuwa ni kumuumiza masikini.

“Kuishi ni gharama, kufa nako kuna ada, jamani, twaelekea wapi sisi? Heri tuchome maiti badala ya kuzika kwa kuwa hatuwezi hiyo gharama,” alisema Lydia Ndinda, mkazi wa Changamwe.

Alisema kuwa gharama ya kuchoma maiti ni nafuu, lakini alimsihi gavana kutupilia mbali ada hizo kuwapunguzia mzigo wasiojiweza katika jamii.

“Hii ni kwa sababu huwa tunashindwa kugharamia bei ya mazishi hapa Mombasa. Itabidi tufanye harambee na hiyo bado ni gharama nyingine mwili ukiendelea kukaa katika chumba cha kuhifadhia maiti. Tunaomba ada hiyo ipunguzwe, maiti hana pesa,” alisema Victor Wesonga, mkazi wa Jomvu.

Alisema kuwa familia zinahofia gharama inayowakodolea macho ya kuwazika wapendwa wao.

“Najua mmeshtuka lakini kumbukeni hatujawahi kuongeza ada hizi tangu ugatuzi. Tumeongeza kwa Sh5000 tu,” alisema Ramla Mohammed, Mkurugenzi wa mapato mjini Mombasa.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →