Skip to main content

Naibu Rais William Ruto Aomboleza Kifo cha Afisa wa Mawasiliano Anthony Kariuki

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 28 September 2019.

Naibu Rais William Ruto amemtaja afisa wa mawasiliano wake Anthony Kariuki kama mtu mwenye bidii ambaye alikuwa amejitolea kwa kazi yake.

Anthony Kariuki alikuwa akihudumu katika kitengo cha mawasiliano katika afisi ya Naibu Rais William Ruto.

Naibu Rais William Ruto alisema kwenye ukurasa wake wa Twitter, "Natoa rambi rambi zangu kwa familia, wafanyikazi wenzake na marafiki wa mfanyikazi wangu Anthony Kariuki. Kariuki alikuwa mchapa kazi, mtu ambaye ungemtegea kwa wakati wowote na aliyejitolea kwa kazi yake,".

Naibu Rais William Ruto alisema pia, "Tutaukosa sana ujuzi wake. Jipeni moyo kwani Kariuki anapumzika mikononi mwa Mungu. Lala salama,".

Anthony Kariuki alifariki baada ya kugongwa na gari alipokuwa akivuka barabara kuingia katika makazi yake mtaani Buruburu mwendo wa nne usiku.

Aligongwa na gari akivuka barabara kuingia alikokuwa akiishi. Alifariki kabla ya kufika hospitalini," alisema mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika afisi ya Naibu Rais David Mugonyi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →