This archive report was first published on 28 September 2019.
Waziri wa Kawi Charles Keter alizuru eneo la Tiaty, kaunti ya Baringo, ambapo alizomewa na Mbunge wa Tiaty William Kamket na baadhi ya viongozi wa kaunti waliomshutumu kwa kuwatenga.
Mradi wa kawi ya mvuke ulikuwa kikwazo kikuu cha mzozo huo, na Kamket alisema kuwa Keter alikataa kujadili kuhusu mradi huo kabla ya kuzuru eneo hilo.
"Shida ingetokea wapi iwapo ungetuarifu ulikuwa unapanga kuzuru eneo hili, hata kwenye simu ulikataa kuwa huna mpango wa kuja hapa wakati nilipokupigia simu. Mbona unafanya hivi, madharau ni ya nini?" Kamket alisema.
Waziri Keter alijitetea na kusema kuwa alizuru eneo hilo kwa ajili ya kujifunza zaidi kabla ya kufanya kikao na viongozi wa kaunti kujadiliana kuhusu mambo ibuka yanayowakumba wakazi.
"Hatujawahi fanya kikao, hii ni mara yangu ya kwanza kuzuru hili eneo. Mbunge wa eneo hili amekuwa akinishurutisha kujadiliana naye kuhusu mradi huu afisini mwangu lakini nilihisi ni vyema nizuru eneo hili mwanzo kabla ya kufanya kikao naye," Keter alisema.