This archive report was first published on 27 September 2019.
Mfanyabiashara Humphrey Kariuki alishtakiwa kwa kukwepa ushuru wa takriban KSh 41 bilioni na kiwanda chake cha Africa Spirits kilifungwa kufuatia tuhuma hizo.
Alipata pigo baada ya mahakama kumzuia kuchukua pasipoti yake, na alisema kuwa alihitaji kuchukua stakabadhi hiyo ndiposa asafiri ughaibuni kushughulikia biashara zake.
Alipewa fursa ya kuingia kiwanda chake Jumamosi na kuchukua noti za zamani za KSh 1,000 ili kuzibadilisha, huku kiwanda cha Africa Spirits Limited kiliiomba mahakama kuruhusu kiwanda hicho kifunguliwe.
Wakili wa kampuni hiyo, Cecil Miller, alisema kuwa ni kejeli kwa serikali kuitisha ushuru wa KSh 150 milioni kila mwezi ilhali milango ya kiwanda hicho imesalia kufungwa.
Aliongeza kuwa hatima ya wafanyikazi zaidi ya 500 haijulikani tangu kufungwa kwa kiwanda hicho.