This archive report was first published on 27 September 2019.
Alhamisi, Septemba 26, 2019, habari zilikuwa zikienea kuwa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Cassie Ventura alifunga pingu za maisha na barafu wake wa moyo Alex Fine.
Wanawake wote ulimwenguni walifurahia habari hizo kwani awali mrembo huyo alikuwa akichumbiana na rapa Diddy kwa miaka 11 bila ya kupata pete ya kuposwa.
Wakati huo huo, bintiye ya Gavana wa Nairobi Mike Sonko, Saumu Mbuvi, aliamua kuzungumzia swala hilo.
Alisema wanawake wanatakiwa kuwa makini sana wakati wa mahusiano ya ndoa.
Aliongeza pia kuvumilia na kuwa na matumaini mwanamume mnyama anaweza kubadilika basi nikupoteza muda.
“Wazo la siku. Cassie alichumbiana na Diddy kwa miaka 11, lakini alikosa kumposa ama hata kumuoa ama hata kuwa na mipango ya kumuoa ama kuwa na familia naye,” alisema mama huyo msimbe.
“Wacha kuwa kwenye uhusiano ambayo mwanamume hakuheshimu. Furaha yako yatakiwa kuja ya kwanza. Mwanamume anayekupenda atafanya kila juhudi kuwa nawe. Ya kesho hatuyajui mbona kukubali kuwa na maisha mabaya?” aliuliza Saumu.
Alisema pia wanawake wanatakiwa kujifunza kuwapenda wanaume wanaowaenzi.
Alisema pia wanawake wanatakiwa kukoma kujilazimisha kwa wanaume ambao hawana hisia yoyote ya mapenzi kwao.