Skip to main content

Makahaba Wafurika Bomet Kuwawinda Wakulima wa Majani Chai

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 26 September 2019.

Makahaba Wafurika Bomet Kuwawinda Wakulima wa Majani Chai

September 26, 2019

Wakulima wa majani chai wa kaunti ya Bomet na Kericho watarajia kupokea bonasi zao karibuni baada ya makahaba kufurika kaunti hiyo.

Wakulima hao wamefanya kazi kwa makundi ya makahaba ambayo yalipata mavuno mazuri kutoka kwa wakulima wa mahindi katika kaunti ya Trans Nzoia.

Maeneo ya biashara ya Silibwet, Mogogosiek, na Kapkwen yameandikisha asilimia kubwa ya kuongezeka kwa biashara kwa sababu makahaba wamepata vyumba katika mikahawa na mahoteli mjini Bomet na viunga vyake.

Mkuu wa polisi eneo la Bomet Central, Musa Imamai Omar, amewaonya wakulima dhidi ya kujihusisha na raha ya muda na kwa hivyo kushauri kuwekeza au kutumia hela zao kwa busara.

Aliwashauri pia dhidi ya kubeba kiasi kikubwa cha hela ili kuepuka kuwindwa na wezi au makahaba hao.

Wakulima wa majani chai wa Bomet na Kericho watarajia kupokea bonasi zao karibuni baada ya makahaba kufurika kaunti hiyo.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →