This archive report was first published on 26 September 2019.
Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i alizuru ngome ya Rais Uhuru Kenyatta katika kaunti ya Kiambu, Septemba 26, 2019.
Aliahidi kukabiliana na genge la wahuni linalohangaisha wakazi wa eneo hilo, huku akiongea eneo bunge la Gatundu.
Waziri Matiang'i aliwataka polisi kufanya oparesheni kali kuwafurusha wahuni wote wanaowasumbua wakazi nyaka za usiku.
Aliwataka pia wakazi wa Kiambu kushiriki taarifa zao za kusisimua na polisi ili kushughulikia hali hiyo.
Waziri huyo aliandamana na mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria wakati wa ziara yake.