Skip to main content

Waziri George Magoha Afuta Leseni ya Shule ya Precious Talents

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 26 September 2019.

Waziri wa Elimu, George Magoha, amefuta leseni ya Shule ya Msingi ya Precious Talents baada ya mkasa wa kuporomokewa kuua maisha ya wanafunzi 8.

Shule hiyo ilikuwa imefungwa kwa wiki moja ili kuruhusu uchunguzi kufanywa kuhusu kisa hicho.

Magoha amewaagiza wanafunzi walioathirika kupelekwa katika shule za serikali zilizoko karibu.

Wanafunzi karibia 800 wa shule hiyo walihamishwa hadi Shule ya Msingi ya Ngong Forest, ambayo itawachukuwa wanafunzi 480, huku 180 wakipelekwa katika Shule ya Msingi ya Jamhuri na wengine 130 wakijiunga na Shule ya Msingi ya Riruta Satellite.

Shule nyingine ambayo imeathirika ni Shule ya Msingi ya Pama Academy katika mtaa wa Kangemi ambayo leseni yake imefutwa kwa sababu ya majengo duni.

Magoha amefichua kuwa Wizara ya Elimu itatoa msaada wa madawati na vitabu kwa wanafunzi hao katika shule zao mpya.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →