This archive report was first published on 26 September 2019.
Michelle Yola, aliyekuwa mchumba wa rapa Prezzo, ametangaza kuwa amejaaliwa mtoto wa pili na mpenziwe wa kizungu mwaka mmoja baada ya kujifungua mtoto wao wa kike.
Yola alipakia picha ya mkono wa mtoto huyo mitandaoni huku akichapisha ujumbe ulioashiria kwamba kwa sasa yuko Paris, Ufaransa.
Alisema kuwa licha ya kwamba alijifungua mtoto huyo awali, alichukua muda kabla ya kuwajulisha mashabiki zake.
"Asanteni nyote kwa jumbe zenu ila sikujifungua huyu mtoto hili juma. Samahani kwa kutowajulisha kwa wakati ufaao," alisema.
Aliongeza, "Nimekuwa na huyu mtoto kwa muda sasa. Hata hivyo asanteni kwa kunionyesha upendo,".
Yola na Prezzo walichumbiana kwa muda na hata kuchanja chale za majina yao kwenye mikono yao.
Alipozungumza na Tuko, Yola alidai kuwa Prezzo alitishia kuiba stakabadhi zake kufuatia kutengana kwao.
Alisema, "Nimekuwa na huyu mtoto kwa muda sasa. Hata hivyo asanteni kwa kunionyesha upendo,".