Skip to main content

Magavana Watoa Mawazo Yao Kuhusu Pendekezo la Raila Odinga la Kuunda Serikali ya Mirengo Mitatu

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 25 September 2019.

Magavana Watoa Mawazo Yao Kuhusu Pendekezo la Raila Odinga la Kuunda Serikali ya Mirengo Mitatu

Magavana wengi wamepinga pendekezo la Raila Odinga la kuunda serikali ya mirengo mitatu, wakisema kuwa itakuwa na madhara kwa nchi.

Walisema kuwa iwapo kutakewepo na mpango wa kuwateua viongozi kulingana na maeneo wanayowakilisha Wakenya, wataumizwa na mzigo zaidi.

Waziri mkuu wa zamani, Kiraitu Murungi, alisema kuwa serikali inapaswa kuimarisha uchumi wa nchi badala ya kuunda nafasi zingine za kazi ambazo zinazingirwa na siasa.

Alisema, "Badala ya kuunda urasimu mwingine, safu nyingine ya kisiasa, cha kutiliwa maanani sasa ni kuzingatia kuboresha viwango vya uchumi nchini jinsi ambavyo kaunti zingine tayari zimeanzisha,".

Raila Odinga alipendekeza kwamba serikali ipanuliwe zaidi kutokana na mfumo wa ugatuzi, na kuwaacha kaunti zisalie jinsi zilivyo.

Alisema kuwa itakuwa bora zaidi iwapo kutakuwepo na mikoa 14 ambayo itahusika katika kusambaza hela kwenye majimbo.

Alisema pia, "Suluhu la kudumu la kukabiliana na utata unaozingira ugatuzi, itatubidi tuketi chini turejelee suala nzima la muundo ambao ugatuzi umefuata,".

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →