This archive report was first published on 25 September 2019.
Mtangazaji Andrew Kibe alifanywa mahakamani Jumatano, Septemba 25, kwa madai ya kukosa kulipa deni la shilingi milioni 2.5.
Kibe alipe deni la shilingi 215,000 ambalo alikuwa amekopa kutoka kwa rafiki wake mmoja miaka saba iliyopita.
Kulingana na runinga ya Citizen, Kibe alichukua deni hilo kutoka kwa rafiki yake na alikuwa alipe na riba ya alfu 55,000.
"Kukosa kulipa deni hilo kufikia Februari 28, 2012 kunavutia faini ya asilimia 7.5 kwenye riba kila siku nne zinazopita bila deni kulipwa," alisema Kibe.
Kwa sasa deni hilo limepanda na kufikia shilingi milioni 2.5 huku Weru akitaka mahakama itoe uamuzi wa Kibe kulipa fedha hizo.
Kibe alishtakiwa mwaka jana na hivyo huenda hata deni hilo limepanda zaidi ya shilingi hizo milioni 2.5.