This archive report was first published on 24 September 2019.
Wabunge wameudhika baada ya mbunge wa Malava Malulu Injendi kutengeneza mswada unaopanua kudhibiti mitandao ya WhatsApp na Facebook.
Msukumo wa mswada huo ni kuhakikisha kwamba wote wanaotaka kuanzisha vikundi kupitia WhatsApp na Facebook watalazimika kutafuta leseni kwanza kwa shirika la kudhibiti mawasiliano nchini (CAK).
Wabunge hawa wameongozwa na Babu Owino, ambaye alisema kuwa mswada huo ni upuzi na huwezi kuwanyima vijana uhuru wao wa kuongea kama walivyohakikishiwa kwenye katiba.
"Huo ni upuzi. Huwezi kuwanyima vijana uhuru wao wa kuongea kama walivyohakikishiwa kwenye katiba," Babu Owino alisema.
Wabunge wengine wameeleza kuwa Wakenya wanafaa kufanya mageuzi ya kikatiba na kubadilisha viti vya ubunge kwani baadhi ya wabunge hawajui wanalofaa kufanya.
Wakati wa kujadili mswada huo, wabunge wameuliza Malulu kutafuta mswada mwingine kwani bunge haliwezi kujadili mswada wa kiwango hicho.