Skip to main content

Marapa Maarufu Wasindikizwa na Waganga kwa Mahojiano ya Redio

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 September 2019.

Wakati wa mahojiano ya redio kwa Clouds FM, marapa maarufu kutoka Tanzania waliamua kuwaajiri waganga kama walinzi wao wa kibinafsi.

Wawili hao walioandamanana na Rostam, iliyobuniwa na wasanii Roma na Stamina, walikuwa na maoni ya kujitolea kwa waganga hao.

''Wajua kila mtu anataka kuwa na mlinzi, utamuona msanii mmoja akiwasili katika hafla fulani na walinzi 20, kwa kazi gani?'', alidai Roma.

Aliongeza kuwa anaamini wanaume wanatakiwa kulindwa ndio maana wakachukua hatua hiyo.

''Kulingana nasi tumeamua kuja na waganga wetu kwa sababu tunawaamini, na tunajua tuko kwa mikono salama,'' aliongezea msanii huyo.

Wakati wa mahojiano, wawili hao walikuwa na waganga wao wakipitia pamoja na walinzi wao.

''Kulingana na kundi hilo, hakuna tofauti kati ya walinzi wa kawaida na waganga hao kwani wote hutoa huduma za usalama,'' ilisema Rostam.

Alishikilia kuwa hawapigani vita vya kimwili bali vya kiroho ndio maana wakawatafuta waganga hao.

Wakati huo huo, hatua yao imeibua hisia mseto miongoni mwa Watanzania huku wengi wao wakiwakashifu kwa kutumia uchawi.

Wengine wao nao walidai kuwa waganga sio wachawi ambao hufanya mazinga umbwe.

Published on September 24, 2019.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →