This archive report was first published on 24 September 2019.
Chama cha upinzani cha FDU-Inkingi nchini Rwanda kimeeleza kuwa mwanasiasa maarufu wa chama hicho, Syridio Dusabumuremyi, ameuawa kwa kudunguwa kisu hadi kufa. Dusabumuremyi alikuwa kazini wakati aliposhambuliwa na wanaume wawili wakiwa katika duka lake la kuuza chakula katika kituo cha afya kilichopo wilaya ya kati ya Muhanga.
Idara ya upelelezi nchini Rwanda imeeleza kwamba Dusabumuremyi alidungwa kisu hadi kufa na watu wasiojulikana. Idara hiyo pia imeeleza kwamba tayari washukiwa kadhaa wametiwa nguvuni huku uchunguzi zaidi unafanywa kubaini lengo la mauaji hayo.
Ingabire anasema mauaji ya Dusabumuremyi ni ya punde zaidi kufuatia msururu wa mashambulio dhidi ya wafuasi wa chama chake kwa lengo la kuwatishia. Kiongozi wa chama hicho, Victoire Ingabire, amesema kwamba mauaji hayo ni ya punde zaidi kufuatia msururu wa mashambulio dhidi ya wafuasi wa FDU-Inkingi.