Skip to main content

DP Ruto Promises New School After Precious Talent Collapse

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 24 September 2019.

DP Ruto Promises New School After Precious Talent Collapse

Naibu wa Rais William Ruto amewahakikisha wakazi wa Dagoretti Kusini kuwa serikali itawajengea shule mpya ya msingi ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule zilizopo eneo hilo.

Alipowasili hospitalini kufuatia kisa kilichotokea katika Shule ya Precious Talent, Ruto alifichua kwamba kuna mipango ya kujenga shule mpya ya serikali.

"Serikali itakusanya rasilimali ya KSh 20 milioni ili kwa muda wa miezi mitatu ijayo tujenge shule ya msingi ya serikali ambayo itakuwa chini ya Shule ya Lenana. Hii itasaidia watoto kupata elimu bora na kupunguza msongamano katika shule zingine eneo hili," alisema Ruto.

Alipewa taarifa kwamba jengo liliporomoka mwendo wa saa 6:50 na kuwanasa wanafunzi ambao walikuwa wakijitayarisha kwa masomo yao ya siku.

Waziri wa Elimu George Magoha alithibitisha kuwa wanafunzi saba walipoteza maisha yao katika kisa hicho huku zaidi ya 64 wakilazwa katika hospitali mabalimbali ambapo wengi wao walikimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kenyatta.

"Wanafunzi saba wamefariki huku 64 wakilazwa katika Hospitali Kuu ya Kitaifa ya Kenyatta. 62 kati yao walikuwa na majeraha madogo. Wawili wakiwa katika hali mahututi," alisema Magoha.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →