Skip to main content

Mazishi ya Tob Cohen: Hatua kwa Hatua

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 23 September 2019.

Mazishi ya Tob Cohen: Hatua kwa Hatua

Mazishi ya Tob Cohen, mwanaharakati wa habari wa Israeli, yatafanyika Jumanne, Septemba 24, 2019, katika makaburi ya Wayahudi jijini Nairobi. Sarah Wairimu, mshukiwa wa mauaji hayo, atahudhuria mazishi baada ya kuruhusiwa na mahakama ya juu.

Desturi za kiyahudi zinafahamisha taratibu za mazishi, ambazo zinajumuisha hifadhi ya maiti, Sinagogi, au makaburini. Kuna taratibu kadhaa ambazo ni bora kuangalia wakati wa kumtayarisha maiti hadi kuzikwa.

Wanaume wanaoshiriki mazishi, hata kama sio Wayahudi, huvaa vitambaa kufunika vichwa vyao. Jeneza halitumiki kwa kuwa inaaminiwa ni kukosa heshima katika itikadi za kiyahudi. Hamna maua kwa kuwa huashiria uhai na hapo shughuli inayofanyika huwa ni kuhusu kifo.

Wakati wa mazishi, familia ya marehemu inahudhuria na kushuhudia. Baada ya maziko, mstari sambamba hutengenezwa na familia ya marehemu kupita katikati ishara ya umoja na wanapopita, watu huwatamkia waombolezaji 'Hamakom Yinachem Et Chem' ambayo kwa kirefu husemwa 'Hamakom Yinachem Et Chem Bitoch Shi Ar Aveilei Tzion Viyerushalayim' kwa maaa ya Mungu akupe utulivu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →