Skip to main content

Bingwa Darek Formella, Afunga Bao la Ushindi Dakika Chache Baada ya Kifo cha Babake

N

Nyakundi Report

Newsroom 2 min read

This archive report was first published on 22 September 2019.

Bingwa Darek Formella, Afunga Bao la Ushindi Dakika Chache Baada ya Kifo cha Babake

Mei 22, 2019 - Mchezaji wa zamani wa Lech Poznan, Darek Formella, alifunga bao la ushindi katika dakika ya 81 ya mechi ya Sacramento Republic dhidi ya Rio Grande Valley FC, huku akiwa na habari kuhusu kifo cha babake.

Formella alishiriki katika mechi hiyo kali, licha ya kupata taarifa za tanzia kuhusu kifo cha babake dakika chache tu kabla ya kuanza kwa mechi hiyo.

Alionyesha uledi wa hali ya juu wakati wa mechi hiyo, huku akifunga bao la ushindi na kuisadia kikosi chake kutwaa ushindi wa 2-1.

Formella alikuwa ameorodheshwa kwenye kikosi hicho hakuwajulisha wenzake kuhusu habari hizo, huku kocha wake akikosea kumpea muda wa kutosha uwanjani.

Alitambulishwa katika kipindi cha pili kwenye nafasi ya Stefano Bonomo, na kuandikisha matokeo ya kuridhisha.

Formella aliweka taarifa hizo kwenye mtandao jamii, akiwafahamisha mashabiki wake kuhusu mechi na pia kifo cha babake.

"Babangu alikuwa akiugua saratani. Masaa matatu kabla ya mechi nilifahamishwa kuwa aliaga dunia," alisimulia mchezaji huyo.

Alisema kuwa alijaribu kutomwambia yeyote kuhusu kilichokuwa kikiendelea, kwa kuelekeza akili zake kwenye mechi hiyo na kujikaza nilivyoweza.

Formella alikuwa na magoti ya wazi kwa hisia zake, huku akifunika uso wake na kuanguka baada ya kufunga bao la ushindi.

Klabu ya Sacramento Republic walimtolea babake Formella risala za rambi rambi, na kumpongeza nyota wao kwa kuonyesha ukakamavu licha ya kifo cha babake.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →