This archive report was first published on 22 September 2019.
Madereva wawili wa Gavana wa Nairobi Mike Sonko wamefikishwa mahakamani kwa madai ya kufunga barabara wakati Rais Uhuru alipita. Hii ilikuwa kwenye barabara ya Mombasa mnamo Agosti 29.
Wawili hao, Antony Wangamba na Joseph Njue, walitekeleza kosa hilo kwa kutumia magari ya V8 na kufunga barabara huku msafara wa rais ukiwa unapita kutoka uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kuelekea Ikulu.
Wawili hao walishtakiwa mnamo Septemba 9 mbele ya jaji wa mahakama ya sheria za barabarani Martha Nanzushi.
Madereva hao walikanusha madai ya kufunga barabara kama ilivyodaiwa na kufunguliwa kwa bondi ya shilingi 50,000 na 100,000 huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena mwezi Novemba.
Wasiwasi wa TUKO.co.ke kujua iwapo wawili hao walikuwa pamoja na mdosi wao wakati wa tukio hilo hazikufua dafu.