Skip to main content

Kabogo: Rais Uhuru na DP Ruto Wanaingia Pamoja, Haiwezekani Kuwatenganisha

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 22 September 2019.

Aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo amewataka viongozi wa Jubilee kuheshimu Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto.

Alisema wawili hao walichaguliwa pamoja na wanaongoza serikali pamoja, kwa hivyo haiwezekani kuwatenganisha.

Alisema hili Jumamosi, Septemba 21, alipokuwa akihudhuria mazishi ya kaunti ya Murang'a.

"Kuwepo kwa Kieleweke na Tangatanga ndani ya chama kimoja linamaanisha kuna tatizo, na hilo hapa kwetu," alisema Kabogo.

Alisema pia kwamba ni lazima viongozi wote washirikiane ili serikali ya Uhuru na Ruto iweze kufanyia wananchi kazi kama ilivyoawaahidi.

"Tunahitaji kusaidia rais na naibu wake kutekeleza waliyowaahidi Wakenya, na hilo litawezekana tu viongozi wakifanya kazi pamoja," alisema.

Aliongeza kwamba Uhuru akikosa kufanya kazi, hatabeba msalaba peke yake, hata naibu wake atakuwa pia amefeli.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →