Skip to main content

Kirinyaga: Majambazi wavamia kanisa na kuiteketeza moto ▷ Kenya News

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 22 September 2019.

Kirinyaga: Majambazi wavamia kanisa na kuiteketeza moto

Majambazi walivamia kanisa la Full Gospel Life Mission, kwa kuiteketeza kwa petroli, Kaunti ya Kirinyaga mnamo Jumamosi, Septemba 21, katika kisa ambacho kimewaacha wakazi vinywa wazi.

Chanzo kilichopelekea majambi hao kuchoma kanisa hilo bado haijabainika.

Wakazi wa Difathas waliuawa na baridi baada ya moto huo kuchoma kanisa hilo na kuharibu mali ya thamani ya KSh 1 milioni.

"Tumepoteza mali thamani ya KSh1 milioni. Hakuna kitu kilichookolewa. Hatukuwahi kujua kuwa mtu anaweza kuchoma mahali pa kumwabudi Mungu," alisema Isaack Kiringa siku ya Jumapili, Septemba 22.

Isaack Kiringa alisema walijaribu kwa masaa kadhaa kuzima moti huo lakini juhudi zao ziliambulia patupu kwani moto huo ulisambaa kila mahali.

"Tulishindwa. Moto ulichoma kila kitu ikiwemo viti na misalaba. Ilikuwa ya kutamausha sana," alielezea pasta huyo huku akiwataka polisi kuanzisha uchunguzi na kuwakamata wahalifu hao.

Polisi wa Kirinyaga Mashariki waliwaomba wakaazi kushirikiana na polisi kuwasaidia katika uchunguzi wao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →