This archive report was first published on 22 September 2019.
Naibu Rais William Ruto alisafiri humu nchini Jumapili, Septemba 22, na kuwasiliana na wakazi wa Embu. Picha: William Ruto
Askofu wa Kanisa Katoliki dayosisi ya Embu Paul Kariuki alisifia ziara za Naibu Rais William Ruto humu nchini akisema ni za kuleta maendeleo.
Alisema Ruto anahakikisha kuwa maendeleo yanawafikia wananchi kwa kutembea na kujua matatizo yao.
"Watu wengine hawataki kuwa nyuki, wanataka kuwa inzi...kazi yao ni kutafuta pale pameoza....alafu wanaambia nyuki eti anatangatanga, haoni ile kazi mzuri nyuki anafanya," alisema askofu Kariuki.
Aliongeza, "Kama vile naibu rais anaambiwa ati anatangatanga, wewe naibu wa rais endelea kutangatanga ukifanya kazi ya Mungu na kufanyia hawa wananchi kazi."
Askofu Kariuki alijitosa kwenye siasa za urais 2022 huku akisuta mrengo wa Kieleweke ambao umekuwa ukimuingilia DP Ruto.
"Wacha 2022 itafiki, hiyo mnasema kieleweke itafika....mtajua hamkuelewa vizuri," askofu alisema.