Skip to main content

IEBC Afisa Mkuu Mtendaji Ezra Chiloba anataka kulipwa fidia ya KSh 52.5 milioni

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 22 September 2019.

Alipofurushwa ofisini mwaka mmoja sasa, katika jumba la Anniversary Towers, Ezra Chiloba, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), amefika kortini akitakata kulipwa fidia ya KSh 52.5 milioni kwa kufutwa kazi kwa njia isiyokuwa halali.

Chiloba, kupitia kwa kesi iliyowasilishwa na kampuni ya mawakili ya Wandabwa, anataka kulipwa fidia kwa kufutwa kazi kwa njia isiyokuwa halali, kama ilivyojadiliwa katika gazeti la Daily Nation la Jumapili, Septemba 22, 2019.

Alidai kuwa njia iliyotumiwa na maafisa wa kuu wa tume hiyo haikuwa halali na pia Chiloba hakupewa nafasi ya kujitetea.

"Madai ya mlalamishi yanakujia kutokana na hatua ya 1EBC ambayo ilikuwa kinyume cha sheria, njia isiyokubalika na pia sio halali ambayo inaweza kulinganishwa na 1. Mapumziko ya lazima 2. kupigwa marufuku na 3. kutamatishwa kwa mkataba wake," ilisoma taarifa hiyo kutoka kwa mlalamishi.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →