Skip to main content

Ndovu Mwenye Upembe Mmoja Avamia Nyumba ya Jamaa na Kula Mahindi Kwenye Magunia

N

Nyakundi Report

Newsroom 1 min read

This archive report was first published on 21 September 2019.

Ndovu mwenye upembe mmoja amevamia na kubomoa paa la nyumba moja kisha kufyonza mahindi yaliyokuwa yamehifadhiwa kwenye magunia.

Wakazi wa eneo hilo wameendelea kulaumu Shirika la Huduma ya Wanyamapori (KWS) kwa kukosa kuwadhibiti ndovu hao hatari.

Wakati ndovu akivamia makazi ya jamaa huyo, inasemekana hakuwapo kwani alikuwa amerauka kwenda kazini.

Wakazi wameendelea kulaumu Shirika la Huduma ya Wanyamapori (KWS) kwa kukosa kuwadhibiti ndovu hao hatari wanaotembea ovyo ovyo na kufanya uharibifu mkubwa na hata kutishia maisha ya binadamu.

“KWS haiwajibiki katika kuwadhibiti ndovu hao. Bila kusahau kwamba hakuna fidia ambayo mkulima hupokea panapotokea uharibifu wa aina hii au wakati mpendwa wao anapouawa na ndovu,” alisema Rodrick Mwachanya, mkulima wa Kamtonga.

Wakati huouo wakazi wamelalama kwamba KWS limekuwa likijikokota sana wakati wanapoitwa kukitokea dharura ya kuvamiwa na wanyama hasa ndovu.

Be the first to react

Support

Support this reporting

M-Pesa support recorded against this story.

Send support →

Stay close

Get the briefing

Major updates by email. No spam.

Get email brief →

Share

Save share card

Download a clean portrait card for sharing.

Save image →